Propellerads
Propellerads
Propellerads
Daily Updates!

We share informations with you

Propellerads

Saturday, 18 February 2017

MWALIMU MKUU AVULIWA MADARAKA KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA UTOAJI WA ADHABU

Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Uyowa Tabora amevuliwa madaraka ya kuwa mwalimu mkuu na kuwa mwalimu wa kawaida kwa kushidwa kusimamia utoaji wa adhabu shulenikwake.

Jumanne mkuu huyo hakuwepo shuleni alienda kwenye semina wilayani na hapo Shuleni kulikuwa na ukaguzi wa usafi kwa wanafunzi na ikabainika watoto wengi wakakutwa wachafu na wamevaa nguo kwa kujaladia(yaani nguo mbili mbili).

 Walimu wakaamuru wakazitoe hizo nguo walizo jaladia na watoto hao wakaadhibiwa na walimu ghafra ikaibuka tafrani toka kwa wazazi wakaja juu karibia kijiji kizima wanataka kuwapiga walimu kwa kuwapiga watoto wao kitendo kile  kilikuwa kizito ikabidi kwa usalama wa wa Walimu wakachukuliwa kwenda kulala kituo cha polisi Ulyankulu.

Jana timu ya Halmashauri walifika hapo shuleni wakiongozwa na Afisa Elimu Msingi, baada ya uchungunzi kukamilika wakamvua madaraka mkuu wa shule hiyo na kuondoka na majina kadhaa ya walimu,mpaka sasa haijafahamika ni adhabu gani zaidi watapewa walimu hao dhidi ya tukio hilo.

0 comments:

Post a Comment

Propellerads