Propellerads
Propellerads
Propellerads
Daily Updates!

We share informations with you

Propellerads

Saturday, 18 February 2017

MKURUGENZI AVUNJA KIKAO CHA MADIWANI MERU

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Meru Bwana Christopher Kazeri kwa masikitiko makubwa na kwa mshangao mkubwa jana alivunja kikao na kuwaamuru wataalam watoke nje ya ukumbi wa halmashauri.

Sababu kubwa ni kushindwa kujibu maswali ya waheshimiwa Madiwani kuhusu kuvurugwa kwa bajeti ya halmashauri na kuacha vipaumbele vya halmashauri na kuingiza vitu ambavyo siyo kipaumbele cha halmashauri kwa sasa.

Kwa mfano amefoji na kuingiza kwenye bajeti ununuzi wa gari la mkurugenzi, ujenzi wa nyumba za wafanyakazi, na ununuzi wa wa pikipiki za watendaji. Hivi siyo vipaumbele vya halmashauri kwa sasa. Sasa alivyobanwa na maswali kuhusu haya ndipo alipoamua kukimbia kikao na kuwaamuru watendaji watoke nje.

Hali hiyo ilipelekea kikao kuvurugika na wajumbe wote kutawanyika na baadhii kukaa makundi makundi wakijadili sintofahamu juu ya Mkurugenzi huyo.

0 comments:

Post a Comment

Propellerads