Propellerads
Propellerads
Propellerads
Daily Updates!

We share informations with you

Propellerads

Saturday, 11 February 2017

MAKONGORO MAHANGA AMPA USHAURI PAUL MAKONDA MKUU WA MKOA WA DAR


WARAKA MFUPI KWA MKUU WANGU WA MKOA, MH. MAKONDA.

Kuna mambo nimejifunza katika utumishi wangu wa umma na kwenye siasa kwa miaka 40 sasa.

Ni kwamba ukipewa cheo:

1. Kwanza, soma na elewa vizuri mamlaka, madaraka na mipaka yako ya kazi kama yalivyo kwenye instruments za kazi yako na sheria na kanuni zilizopo, na kila siku fanya kazi kwa kuzingatia hayo tu.

2. Pili, pamoja na umuhimu wa kujiamini kwenye utendaji wako, usitumie dharau, majivuno, kiburi na much-know.

3. Tatu, hata kama aliyekuteua au boss wako ni rafiki yako sana, anakusifu na kukupongeza sana, na hata kukupa maagizo yanayokiuka mamlaka yako na sheria zilizopo, lazima ujiongeze ili usitoke kwenye misingi niliyoeleza kwenye namba moja na mbili hapo juu.

Kwa maoni yangu wewe Mkuu wangu wa Mkoa, hujazingatia hizo kanuni za utumishi bora, na ona sasa... wanamichezo na wasanii wanakupinga, wanasiasa na wabunge wa chama tawala na wa upinzani wanakupinga, mawaziri wanakupinga, watumishi wa Mungu wanakupinga, wanasheria wanakupinga, Spika anakupinga, watumishi wa chini yako wanakupinga na sisi wananchi tulio wengi tunakupinga....

....Na kipindi hiki aliyekuwa anakupa ujeuri kutokana na namba tatu hapo juu, atakutosa... na hii ni kwa sababu hukufuata misingi ya namba 1 na 2 hapo juu, na pia hukujiongeza hapo kwenye namba 3 ..... Hakika atakutosaaa kama vile hakujui.. ndivyo walivyo mabosi... chunga maneno yangu haya...

Kwa hisani ya Makongoro Mahanga

NAFASI YA MASOMO NCHINI INDONESIA,USIKOSE FURSA HII ADHIMU


http://darmasiswa.kemdikbud.go.id.

MCHUNGAJI GWAJIMA AMEACHIWA TOKA KITUO KIKUU CHA POLISI BAADA YA MAHOJIANO


Mchungani wa Kanisa la uzima na ufufuo almaarufu Gwajima ameachiwa leo toka Polisi baada ya kuripoti toka juzi ambapo alifanyiwa mahojiano na uchunguzi ukihusisha nyumba yake pamoja na mwili wake kubaini kama aliwahi kutumia au anatumia
Baada ya kuachiwa waumini wake wamekusanyika kwa wingi wakisubili kwa pamoja kesho Jumapili anaweza kuhudhuria na kuongoza misa Kanisani

BARAZA LA MITIHANI LATANGAZA KUTOA MTIHANI KWA WANAFUNZI WOTE WA KIDATO CHA KWANZA NA WATAKAOFAULU WATAENDELEA NA WATAKAOFELI KUONDOLEWA SEKONDARI


Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesema kuwa wanafunzi ambao walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za serikali nchini wanahitajika kufanya mtihani wa udahili tarehe 28 mwezi huu na wale watakaofaulu wataruhusiwa kujiunga na kidato hicho.

Taarifa hii ilitolewa kwa mara ya kwanza na Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde lakini kwa mujibu wa barua kutoka NECTA iliyosainiwa na Edgar Kasuga kwa niaba ya Katibu Mkuu kwenda kwa Makatibu Tawala wote wa Tanzania Bara siku ya Jumatatu, wale ambao hawatafaulu hawataruhusiwa kuendelea na masomo hayo ya sekondari.

NECTA inakusudia kutumia mtihani huo kuhakiki uwezo wa wanafunzi waliounesha katika kiwango chao cha ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Msingi uliofanyika mwaka jana. “Watakaofeli  hawataruhusiwa kuendelea na masomo,” inasomeka sehemu ya barua hiyo. Makatibu Tawala wote, maafisa elimu na walimu wakuu wote wa shule za sekondari za serikali waliombwa kufikia leo wawe wamewasilisha orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule zao ili maandalizi yafanyike.

Afisa mmoja wa NECTA amesema maandalizi kwa ajili ya mtihani huo yanaendelea na kwamba wanafunzi  wajiandae. “Maandalizi yanaendelea vizuri na tutatoa taarifa kwa umma kuhusu mabadiliko yoyote yatakayojitokeza,” alisema.

Katika Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Msingi uliofanyika mwaka jana, watoto 789,479 waliofanya mtihani huo ambapo wanafunzi 555,291 walifaulu. Idadi hii ya waliofaulu ni sawa na asilimia 70 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani huo.

Propellerads