Wananchi waliojichukulia sheria mikononi wamechoma nyumba ya mama mmoja eneo Mbalizi mkoani hapa, akituhumiwa kufukua maiti ya mwanawe, kuiogesha na kuihifadhi ndani nyumbani kwake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari amethibitisha kushikiliwa kwa mwanamke huyo.
Amesema tukio hilo linalohusishwa na imani za kishirikina limetokea katika Mtaa wa Shigamba, Kata ya Mbalizi.
Amesema tukio hilo linalohusishwa na imani za kishirikina limetokea katika Mtaa wa Shigamba, Kata ya Mbalizi.
Inadaiwa baada ya mtoto wake kufariki dunia, mama huyo aliamini angefufuka siku ya tatu, jambo ambalo halikutokea hivyo aliamua kwenda kufukua kaburi na kumtoa.

0 comments:
Post a Comment