Propellerads
Propellerads
Propellerads
Daily Updates!

We share informations with you

Propellerads

Saturday, 18 February 2017

KIJANA AZALISHA UMEME KWA MAJI YA MFEREJI PIA AGUNDUA TREKTA KWA INJINI YA PIKIPIKI

Kijana mmoja jina Jackson Mungule mkazi wa Arusha amefanikiwa kuzalisha umeme kwa maji ya mfereji na kuusambaza kwa watu zaidi ya 100. Teknolojia hii ameigundua tokana na tafiti zake ndogo ndogo alizokuwa akizofanya kwa muda mrefu maana yeye kwa muda wote wa maisha yake amekuwa ni mtu mtundu anayejihusisha na mambo ya injini za magari,pikipiki na hata umeme.

Pia anazalisha umeme kwa kutumia kinyesi cha mifugo.
Katika hatua nyingine bwana Mungule amefanikiwa kutengeneza trekta kwa kutumia injini ya pikipiki ambayo inatumia mafuta kidogo hivyo kuweza kuwa mkombozi kwa wakulima.

Ugunduzi huu unaweza kuwa hatua moja muhimu sana katika kuitafuta ile Tanzania ya viwanda ambayo imekuwa ikihubiriwa mara kwa mara na serikali hii ya awamu ya tano ya Dr John Pombe Magufuli,kwani hii inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa sana katika maendeleo ya shughuli na viwanda na kilimo,mfano kwa sasa ka teknolojia hiyo ya Trekta ikiendelezwa inaweza kuwa msaada mkubwa sana kwa wakulima mkoani Arusha ikibidi hata na Tanzania kwa ujumla kwani inaokoa sana matumizi ya mafuta.

Mgunduzi huyu anaomba serikali imsaidie ili aweze kuongeza ujuzi wake zaidi na kuleta tija kwa taifa hii linaweza kuwa jambo zuri na jema sana hasa katika mapambano ya kuondoa ukosefu wa ajira na hata kuongeza kipato na uchumi wa nchi kwa ujumla.

0 comments:

Post a Comment

Propellerads