Mamlaka katika baadhi ya maeneo nchini Indonesia wamepiga marufuku wanafunzi kusherekea siku ya wapendanao wakisema sherehe hizo zinachochea vijana kujihusisha na vitendo vya ngono kiholela. Hayo yamesemwa kuwa badala ya watu kuitumia siku hiyo kukaa na familia na hata kuwakumbuka wale wawapendao walio wengi hutumia katika kufanya ngono zembe.
Katika mji wa Makassar polisi walivamia majumba ya starehe na kuharibu mipira ya 'Condom' iliyowekwa kwa wazi.
Meya wa mji huo alisena kwamba mipira ya 'Condom', iliondolewa maeneo ya wazi baada ya wateja kulalamika na kusema inapatikana lakini haiwekwi wazi.
Katika mji wa pili mkubwa wa Surabaya, wanafunzi wameonywa dhidi ya kusherekea siku ya wapendanao na maafisa wa serikali ambao wamesema sherehe kama hiyo ni kinyume cha maadili ya jamii kwa sababu haipo katika kukuza na kuendeleza maadili ya jamii badala yake inadumaza na kuporomoa maadili.





0 comments:
Post a Comment