Propellerads
Propellerads
Propellerads
Daily Updates!

We share informations with you

Propellerads

Tuesday, 14 February 2017

MTU MZITO ZAIDI DUNIANI APELEKWA INDIA KWA UPASUAJI

Mwanamke raia wa Misri, ambaye inasadikika kwamba ndiye mwenye uzani wa juu zaidi duniani, amewasili mjini Mumbai nchini India kufanyiwa upasuaji.
Eman Ahmed Abd El Aty mwenye umri wa miaka 36 ana uzani wa kilo 500 na anahitaji kufanyiwa upasuaji kumsaidia kupunguza uzani wake.

Safari hiyo ya Jumamosi ilikuwa mara yake ya kwanza kwake kuondoka nyumbani katika kipindi cha miaka 25.
"Eman aliyesafiri kwa ndege ya EgyptAir aliwasili katika uwanja wa ndege wa Mumbai majira ya saa kumi alfajiri na akafika hospitalini Saifee mwendo wa saa kumi na mbili alfajiri. Kitanda maalum alicholalia kiliinulia, yeye akiwa bado kitandani, kwa kutumia kreni," madaktari walisema.

0 comments:

Post a Comment

Propellerads