Marekani imekanusha kuushambulia msikiti wa Omar Ibn al-Khattab,mjini Aleppo nchini Syria,ambapo imedaiwa na wanaharakati kuwa makumi ya watu, wengi wao wakiwa ni raia wameuawa.
Katika taarifa yake,wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon,imesema,shambulio lake lililenga mkutano wa Alqaeda,jirani na msikiti huo,ambapo taarifa hiyo imeambatana na picha ya msikiti wa Omar Ibn al-Khattab,iliyochukuliwa si chini ya dakika tano baada ya shambulio hilo,ukiwa salama.
Wanaharakati wa upinzani nchini Syria,wamedai kuwa takribani watu 40 wameuwa katika shambulio hilo kwenye kijiji cha al-Jinah,walilodai kutekelezwa na Marekani Alhamisi wiki hii.
Aidha wanaharakati hao wamedai watu 250 walikuwa ndani ya msikiti huo kwajili ya ibada husika na kwamba ibada ya Ijumaa,imelazimika kusitishwa kufuatia tukio hilo.






0 comments:
Post a Comment