Hata hivyo, mzozo ambayo ulisababisha mgomo haukupatiwa ufumbuzi, amesema Dk Ouma Oluga, mkuu wa chama cha madaktari nchini Kenya.
Chama cha madaktari kikiongozwa na mwenyekiti wake Oroko Samuel, kuliungana na Waziri wa Afya Cleopha Mailu kwenye ofisi za magavana wakati wa kutiwa sahihi makubaliano hayo.
Makubaliano hayo yalitiwa sahihi mbele ya viongozi wa kidini.
Madaktari walikua wakidai utekelezaji wa mkataba uliosainiwa pamoja na serikali mwaka 2013. Mkataba huo unaeleza kwamba mshahara wa sasa unapaswa kuongezwa mara tatu.
Makubaliano pia yalipanga kuwaajiri madaktari zaidi na kutoa vifaa bora kwa hospitali za umma.
Katika miezi ya hivi karibuni, majaribio kadhaa ya kumaliza mgomo yalishindwa.
Madaktari 5,000 wa sekta ya umma walishiriki katika mgomo huo.
Hospitali nchini Kenya zilikua zimeanza kuwafuta kazi madaktari wanaogoma na kuwaondoa kutoka nyumba zao.
Huduma kwenye hospitali za umma zilikua zimetatizika kutokana na mgomo ambao ulianza mwezi Disemba, huku madaktari na wahudumu wengine wa afya wakitaka mshahara zaidi na mazingira bora ya kufanya kazi.
Itafahamika kwamba serikali ya Kenya ilikua ilipeleka madaktari wa kijeshi kwenye hospitali kubwa zaidi nchini humo ya Kenyatta, baada ya madaktari wa mwisho 300 waliokuwa wakifanya kazi kujiunga na mgomo uliokua ukiendelea nchini kote.






0 comments:
Post a Comment