Waumini katika kanisa la Anglikana huko Bomano Sengerema wameamua kumshushia kipigo Mchungaji Joseph Kwangu,aliwasiri hapo asubuhi walimpokea kwa kipigo na kumzuia kuingia ndani ya kanisa hilo
Baadhi ya waumini wamesema amekuwa akirusha maji ndani ya Kanisa ambayo wamesema hawajui anayatoa wapi,pia wamelalamika kuwa waumini wamekuwa wakimhoji kuwa ibada hizo zinaendana na andiko gani la biblia.
Waumini wamesisitiza kuwa hawawezi kumruhusu Mchungaji huyo kurudi tena aje kusalisha kanisani hapo,na yeye mwenyewe baada ya kuulizwa alisema hayo mambo hayo hayajui na ilimlazimu siku hiyo aondoke kurudi nyumbani.
Baada ya tafrani hiyo Mchungaji mwingine aliruhusiwa kuongoza misa siku hiyo ya Jumapili na ibada ikakamilika kama kawaida.
Tuesday, 21 February 2017
WAUMINI WAMPIGA MCHUNGAJI HUKO SENGEREMA KWA KUONGOZA MISA KWA ISHARA ZA FREEMASON
Unknown
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment