Propellerads
Propellerads
Propellerads
Daily Updates!

We share informations with you

Propellerads

Tuesday, 21 February 2017

KIONGOZI WA UPINZANI RWANDA AUNDA SERIKALI MBADALA

Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, ametangaza kuunda serikali sambamba na utawala uliopo Rwanda, lakini utakaokuwa ukifanya kazi nje ya nchi.
Thomas Nahimana ambaye ni kasisi wa zamani anayeishi nchini Ufaransa ametangaza kuunda serikali hiyo itakayofanyia kazi uhamishoni.
Katika mazungumzo na BBC, mwanasiasa huyo anasema lengo la serikali yake ni kuiondoa madarakani serikali ya rais Paul Kagame, anayemlaumu kuvunja sheria na kukandamiza wananchi.
Thomas Nahimana, amekatazwa kuingia Rwanda kujiandikisha kama mgombea wa kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Baraza lake la mawaziri

Ametangaza tayari baraza lake la mawaziri.
Baadhi ya aliowataja katika baraza lake la mawaziri ni wafungwa wanaotumukia vifungo vya jela nchini Rwanda kwa makosa kama vile kukanusha kuwa mauwaji ya kimbari hayakufanyika nchini Rwanda mwaka 1994.
Bwana Nahimana, ambaye ni mhutu, amelaumiwa kwa kuandika taarifa kadhaa za kikabila na kumkosoa rais Paul Kagame.
Chama chake cha Ishema, bado hakijaandikishwa nchini Rwanda.

0 comments:

Post a Comment

Propellerads