Propellerads
Propellerads
Propellerads
Daily Updates!

We share informations with you

Propellerads

Monday, 20 February 2017

INIESTA AMTETEA KOCHA ENRIQUE

Barcelona, Hispania. Nahodha wa Barcelona, Andres Iniesta amesisitiza kuwa wachezaji wenzake bado wanaimani na kocha wao Luis Enrique.
Macho yote yalikuwa kwa Luis Enrique wakati Barcelona ikipata ushindi kwa tabu wa mabao 2-1 dhidi ya viponde Leganes juzi.
Luis Enrique alizomewa na mashabiki wa Barca wakati timu yake iliponyukwa mabao 4-0 na Paris Saint-Germain katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa hatua ya 16 bora.
Lakini Iniesta amepiga kuwa kuna tatizo na Luis Enrique, akimini kuwa mabingwa hao wa Hispania watarejea katika mstari wao wa ushindi.
"Hatujapoteza kujiamini sisi wenyewe au kocha wetu," alisema Iniesta, ambaye aliingia akitokea benchi dakika 10 kabla ya mpira kumalizika.
"Nafikiri hiki ni kipindi kigumu ambacho tunapita. Naamini tutarudi katika hali yetu ya kawaida ya ushindi.
Lionel Messi alifunga mabao mawili kwenye Uwanja wa Camp Nou na kuwafanya Barca kuwa nyuma kwa pointi moja kwa mahasimu wao Real Madrid wenye mechi mbili mkononi

0 comments:

Post a Comment

Propellerads