Balozi wa Urusi Vitaly Churkin aliyekuwa akiiwalilisha nchi yake ya Urusi Umoja wa Mataifa kwa muda sasa ameripotiwa kuafariki dunia leo ambapo alianguka ghafla kwenye ofisi yake ya Umoja wa Mataifa iliyoko Marekani na kupelekwa hospitali lakini chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika.
Amekuwa mtu muhimu sana hasa katika kutafuta usalama wa dunia hasa kwa kuzitetea nchi Mashariki au zisizofuata mfumo wa Kibepari.
Pia amefanya kazi kubwa sana na yenye weredi hasahasa pale ambapo alisaidia kuzuia nchi ya Syria isivamiwe kijeshi kwa kutumia kura ya VETO. Alishawahi kusema kwamba siku dunia ikitoa Kura ya VETO basi Umoja wa Mataifa utageuzwa kuwa Uwanja wa Fisi kwa Marekani.
Mwaka juzi alipinga maoni yaliyotaka mataifa kama Ujerumani na Brazil kupewa kura ya VETO. Mara nyingi kutokana na hoja zake alijikuta kwenye kashikashi nzito na Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa, mama Samantha Smith kwani kwa kiasi kikubwa alikuwa akipinga vikali sana matakwa ya NATO na Magharibi kwa ujumla.
Kinachoshangaza sana kuhusu bwana Vitaly Churkin ni kuwa amezaliwa Tarehe 21 February 1952 na amefariki tarehe 20 February 2017.
Hivyo kesho ndiyo ilikuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa. Hivi majuzi alionekana akiwa anaongea na mwenye afya njema kabisa,Bwana ametoa Bwana ametwaa,jina lake lihimidiwe,Amina!!
Monday, 20 February 2017
BALOZI WA URUSI UMOJA WA MATAIFA AFARIKI DUNIA
Unknown
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment