Propellerads
Propellerads
Propellerads
Daily Updates!

We share informations with you

Propellerads

Thursday, 9 March 2017

Winnie Mandela alazwa Hospitali Afrika kusini


Shujaa aliyepinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Winnie Madikizela-Mandela, amelazwa hospitalii kwa kile kinachotajwa kuwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya.

Familia yake inasema kuwa alipelekwa hospitali ya Milpark mjini Johannesburg.
Mwezi Disemba mwaka uliopita, Bi Madikizela-Mandela alilazwa hospitali hiyo lakini kile kilichosababisha alazwe hakikutajwa.


Msemaji wake Victor Dlamini, alimwambia mwandishi kuwa alikuwa ameenda kufanyiwa uchunguzi wa kawaida lakini madaktari wakaamua kumlaza.

Bi Madikizela-Mandela alikuwa mke wa Nelson Mandela, na alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi kusajiliwa kama mhudumu wa kijamii nchini Afrika Kusini.

0 comments:

Post a Comment

Propellerads