Propellerads
Propellerads
Propellerads
Daily Updates!

We share informations with you

Propellerads

Thursday, 9 March 2017

Waziri Nape asisitiza waandishi kutumia maarifa yao vizuri


WAZIRI wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ametembelea kituo cha radio cha Efm na kuzindua urushwaji wa matangazo kwa mikoa tisa.

Waziri Nape alifanya ziara hiyo akiongozana na Mkuu wa Idara Habari Maelezo, Hassan Abbas, pamoja na maofisa wengine wa wizara ambapo aliwataka watangazaji hao kuzingatia weledi katika kufanya kazi zao.

Alisema kuwa serikali kwa kutambua mchango wa radio hiyo katika kufanya kazi zake za kiutangazaji pamoja na maendeleo kwa jamii nzima kwa ujumla, ndio maana imewapatia kibali cha kusikika mikoa yote hiyo.

Alisema, kwa miaka mitatu ambayo radio hiyo imekuwa hewani iliwafikia wananchi wengi huku ikijihusisha na masuala mbalimbali ya kijamii.

Alisema kuwa serikali itaendelea kuwa karibu zaidi na radio hiyo na hasa katika kuhakikisha kuwa inaisaidia kusambaa nchi nzima na kukemea watu ambao wanaonekana kuwa na lengo la kuikwamisha.

“Yaani nyie wafanyakazi wa hii radio kwa muda mfupi mmefanikiwa kufanya makubwa kwenye tasnia hii kwa kuwa mmekonga nyoyo za watanzania kutokana na umahiri wenu wa kibunifu, sasa sio watu wanawaparamia tu na kutaka kuwavuruga wakati mmetumia nguvu kujipanga,” alisema Nape.

Kwa upande Mkuu wa Mawasiliano wa radio hiyo, Dennis Sebo alimuomba waziri huyo kufanikisha upatikanaji wa semina za muda mfupi kwa watangazaji nchini ili kuendeleza weledi wa utangazaji huku akiipongeza TCRA kwa kuiwezesha radio hiyo kupata semina mbalimbali.

Efm ambayo imekuwa ikisikika kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, kwa sasa itakuwa ikisikika kwenye mikoa ya Mwanza, Tabora, Tanga, Mtwara, Kigoma, Mbeya, Kilimanjaro pamoja na wilaya ya Babati mkoani Manyara.

0 comments:

Post a Comment

Propellerads