Propellerads
Propellerads
Propellerads
Daily Updates!

We share informations with you

Propellerads

Saturday, 11 March 2017

Lema asema hakuna wa kuogopwa hata kama ni Magufuli


MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amewataka wananchi wa Jimbo hilo kuacha woga na waamshe mori ya kupigania haki ikiwamo kuirejesha Arusha ya Mwaka 2010.

Lema aliyasema hayo jana wakati akiwahutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro mjini hapa

Katika mkutano wake huo wa kwanza tangu alipotoka mahabusu ya Gereza la Kisongo alikokaa kwa miezi minne kutokana na kukosa dhamana ya kesi ya uchochezi inayomkabili, Lema alisema, umefika wakati wa kupigania haki pale inapovunjwa na viongozi akiwamo Rais John Magufuli.

“Hatutaogopa kumkosoa Rais Magufuli pale atakapokuwa amevunja Katiba ya nchi, tutasema kweli na tutapigania haki hiyo,” alisema Lema na kuongeza:

“Wananchi wa Arusha mmekuwa waoga amsheni mori ya kupigania haki. Nawaambieni hivi hakuna mtu aliyetupa nchi vizuri na kirahisi kama Rais Magufuli.

“Nawaambieni kila aliyetakiwa kukemea uovu na hakufanya hivyo ipo siku uovu huo utamrudia. Leo hii huko tunakoelekea hata hao watachoka na watarudi kuimba wimbo tunaoimba sisi,” alisema Lema.

Akielezea kuhusu kukaa kwake mahabusu miezi minne Lema aliyekuwa akishangiliwa kila alipozungumza alisema, wito wa uongozi na kuwatumia wananchi ndio uliomsukuma kukaa magereza.

“Nimekosa dhamana kwasababu ya wito, nisingekuwa na wito wa kuwatumikia wananchi nisingikwenda magereza. Mimi sijaingia kwenye uongozi kwa ajili ya kutafuta fedha,” alisema Lema.

MAISHA YA MAHABUSU

Akizungumzia maisha yake ya mahabusu ambako alipata cheo cha kuwa Mnyampara, alisema mahabusu si kubaya japokuwa roho inaendelea kumuuma kwa wale aliowaacha wakikabiliwa na mateso makubwa.

“Jumatano iliyopita nilirudi Magereza kutafuta ndoo yangu niliyokuwa nakalia nilienda kuichukua na kuiweka chumbani kwangu. Mke wangu aliniuliza nikamjibu kuwa wapo watu wengi walioonewa hivyo kila ninapokuwa nikiomba naiangalia ndoo ile na kuwaombea waliopo magereza.”

"Nimekaa mahabusu miezi minne sina kosa kabisa,nilichukuliwa Dodoma na Polisi usiku nikapelekwa Kondoa, katikati ya njia nikaomba kujisaidia haja ndogo polisi wakanizunguka na silaha za SMG 5 niliwauliza mnanitafuta mimi ama kuna mwingine mnamtafuta niliwaambia kama kuna kitu nimeshau kwenye maisha yangu ni hofu na woga,"

 “Tuliingia Arusha Saa 12 asubuhi nikasikia Mkuu wa Upelelezi Mkoa (RCO) akipigiwa simu na kutoa maelekezo mtu yeyote asinione, nimeanza kukaa mahabusu tangu Mwaka 2004. Lakini nikafikiria nimefanya nini, kuona maono ndiyo yananitesa mimi hivi, neno la Mungu?”, alihoji Lema.


Alisema alipokuwa mahabusu alikuwa akisali na kumuuliza Mungu mbona anateswa wakati yeye ndiye alimpa kauli hiyo,Mungu akamjibu hateseki na akitoka awasamehe na wasubiri kisasi cha Mungu hivyo anasubiri kisasi cha Mungu na anatarajia kumuona Mungu.

KATIBA

Akielezea kuhusu suala la Katiba, Lema alisema Rais Dk. Magufuli akiwa anaapa aliishika pamoja na Biblia akiapa kuilinda na kuitumikia lakini hivi sasa haisimamii.


Huku akinukuu maandiko ya Biblia kutoka Kitabu cha Isaya 30:9-10; “Kwa maana watu hawa ni waasi,watoto wasemao uongo,watoto wasiotaka kuisikia sheria ya bwana,wawa ambiao waonaji,msione na manabii msitoe unabii wa mambo ya haki,tuambieni maneno laini,hubirini maneno yadanganyayo".


Alisema yeye amevaa kombati hivyo aliyosema aliona maono na badala yake watu wengine walidhani amevuta bangi. Hata hivyo kwa vile alitamka neno la Mungu na kisha kuwekwa ndani aliahidi kuendelea kujitetea kwa neno la Mungu na kuthibitisha maono yake.

POLISI

Lema aliwataka polisi kuzingataia sheria na kuacha  kuonea watu kwani wanaishi mitaani hivyo wananchi wakiamua kulipiza kisasi itakuwa jambo lisilopendeza.

Alisema anaomba Mungu hilo lisitokee  lakini ipo siku wananchi  hao watachoka na uonevu huo.

"Polisi mnaona sifa mlisema kazi ya Jamhuri ni kuona watu wanateseka ndiyo maana mnanitesa mimi,polisi hii dhuluma mnayofanya ya kudhalilisha watu, Afrika Kusini ilikuwa na polisi wabaya kuliko ninyi,hao watu mnaozuia wasifanye mkutano iko siku wa

0 comments:

Post a Comment

Propellerads