Propellerads
Propellerads
Propellerads
Daily Updates!

We share informations with you

Propellerads

Sunday, 12 March 2017

Gwajima amtaka Sirro na DPP wamshitaki Makonda


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ametaja makosa ya kisheria yaliyomfanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda kukimbilia Afrika Kusini.

Akizungumza leo kanisani kwake, Ubungo, jijini hapa, Gwajima alidai  kosa la kwanza la Makonda ni kughushi cheti ambacho kinaonyesha yeye ni Paul Makonda wakati akifahamu kuwa yeye ni Daudi Bashite.

“Kosa hilo kwa mujibu wa Gwajima ni kifungo cha miaka saba.Kosa jingine ni kula kiapo cha ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa akisema yeye ni Makonda wakati akijua yeye ni Bashite,” alisema

Gwajima alisema  kosa la hilo la kula kiapo na cheti feki  ni kifungo cha miaka mitatu.

Kosa jingine  alisema ni kupokea mshahara na posho kwa jina la Makonda wakati akifahamu si yeye   na kuongeza kuwa kosa hilo likithibitika atatakiwa kurudisha mishahara na posho zote alizochukua.

Katika kutoa ufafanuzi zaidi amewaomba Kamanda Sirro na Mwendesha mshitaka wa serikali DPP wafanye utaratibu wa kumsaka kokote aliko na waje kumshitaki kwa kosa alilolifanya maana itakuwa ni kulea watu wengine na wengine kuwapeleka jera,amesema Makonda ajitokeze na awe tayari kujibu mashtaka yatakayokuwepo dhidi yake.

0 comments:

Post a Comment

Propellerads