Simba imekuwa timu ya kwanza kufuzu wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC),kwa kuichapa African Lyon kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji Laudit Mavugo alifunga bao pekee la Simba katika dakika 58, akiunganisha pasi iliyopigwa na Ibrahimu Ajib.
Katika mchezo huo kipa wa Lyon, Rostand Youthe pamoja na hali ya unyevu wa Uwanja wa Taifa alifanya kazi kubwa kuinusuru timu yake na mvua ya mabao.
Rostande alifanya kazi ya ziada katika dakika ya 17, 33 na 34 kuokoa mashuti ya Juma Luizio, Said Ndemla na Ibrahim Ajibu kuinyima Simba mabao.
Simba ilifanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi chake kilichoibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Prisons.
Kocha wa Simba, Joseph Omog aliwaanzisha Abdi Banda na Jonas Mkude ambao hawakuanza kwenye mechi ya Prisons.
Kama ilivyotarajiwa, mechi hiyo haikuwa na mashabiki wengi jambo lililofanya viti vingi uwanjani vibali tupu.
Thursday, 16 February 2017
SIMBA YAICHAPA AFRICAN LYON NA KUFUZU ROBO FAINALI
Unknown
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment