Idara ya Polisi nchini malaysia inasema kuwa inawatafuta zaidi ya washukiwa wanne kutoka Korea Kaskazini kuhusiana na mauaji ya kakake wa kambo, Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Kim Jong-nam, alifariki muda mfupi baada ya kupuliziwa sumu katika uwanja wa ndege mjini Kuala Lumpur, juma lililopita.
Polisi wamewatambua washukiwa wanne wote wanaume wenye umri kati ya miaka 43 hadi 47, ambao wanasemekana tayari wameondoa Malaysia.
Watu wanne wanazuiliwa korokoroni kuhusiana na mauaji ya Kim, akiwemo mwanamke ambaye anasemekana kuwa alihadaiwa kutekeleza mauaji hayo.
Polisi wanajaribu kuwatafuta jamaa ya mhasiriwa ili kusaidia katika uchunguzi.
Marehemu Kim Jong-nam, alitarajiwa kutawala Korea Kaskazini, lakini walikosana na babake marehemu Kim Jong-il lakini akaamua kukimbilia uhamishoni.






0 comments:
Post a Comment