Propellerads
Propellerads
Propellerads
Daily Updates!

We share informations with you

Propellerads

Thursday, 16 February 2017

PROF.KITILA MKUMBO ASEMA DR MWAKYEMBE AMEMSAIDIA LISSU

Kwa mujibu wa bandiko lake katika mtandao wa kijamii wa Twiter Profesa Kitila Mkumbo amesema Dr.Harrison Mwakyembe kwa kitendo chake cha kuutangazia umma kuwa wataifuta Tanganyika Law Society(TLS) kwa kujihusisha na siasa,kitendo hiki kimempa umaarufu zaidi mwanasiasa Tundu Lissu kwani kwa mujibu wa Tangazo lile la Mwakyembe mtu aliyekuwa akimlenga alikuwa ni Lissu japo pia hata kuna jina jingine la mwanasiasa Lawrence Masha ambaye kwa hali yake ya kisiasa si maarufu kama alivyo Lissu.

Mkumbo kitendo hiko kimemrahisishia sana Lissu katika harakati zake za kuukwaa uongozi ndani ya Chama hiko cha Wanasheria hapa nchini.

Suala hili limemfanya Lissu kujulikana vizuri zaidi kwa wajumbe wa uchaguzi ule pia Mkumbo akawatakia uchaguzi mwema wajumbe wote wa TLS.

Kwa upande mwingine Tundu Lissu amesema hakuna kiongozi yeyote wa serikali mwenye mamlaka ya kuifuta TLS kwa sababu ipo hapo kwa mujibu wa Sheria,taratibu na kanuni zote za nchi,jaribi hilo hilo lilishawahi kutaka kufanyika kwa viongozi wengi waliopita lakini halikuweza kutokea kwa kuwa ni kitu kigumu mno.

0 comments:

Post a Comment

Propellerads