Mkazi mmoja wa mtaa wa Ushirika ameuawa na jamaa mmoja aliyejulikana kwa jina la Mihambo,mtu huyo alienda shambani kwa ajili ya kupalilia shamba lake na akakutana na huyo mtu aliyemuua alimkatakata kwa mapanga na kupotea uhai.
Polisi wamesisitiza utawala wa sheria ufuatwe na baadhi ya majirani wameomba utaratibu ufuatwe kuliko zile zama za mtu kukamatwa na baada ya siku mbili mnamuona mtaani akitamba kwani hiyo imekuwa ikirudisha nyuma juhudi za ushirikiano baina ya Polisi na raia. Majirani wamedai Mzee huyo aliyeuawa alikuwa ni mtu mzuri ambae hakuwa na tatizo lolote na alikuwa akitumiwa na majirani hao kwa ushauri na huduma ndogo ndogo.
Polisi wamesema taratibu za mashtaka zinaandaliwa na zikikamilika muda wowote mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kwani mpaka sasa anashikiliwa ndani kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
Friday, 17 February 2017
MMOJA ACHINJWA HUKO NZEGA KWA UGOMVI WA ARDHI
Unknown
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment