Viongozi wa ngazi ya juu wa kidunia, wanadiplomasia na maafisa wa masuala ya ulinzi wanakutana kwa mara ya kwanza na maafisa wa utawala mpya wa Marekani chini ya Rais Donald Trump mjini Munich.
Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence, waziri wa ulinzi Jim Mattis na waziri wa nchi hiyo wa mambo ya ndani John Kelly wanaoongoza ujumbe wa Marekani katika mkutano unaohusu masuala ya ulinzi unaoanza leo mjini Munich, Ujerumani.
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Rais wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk, na Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, ni miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kushiriki mkutano huo ambao unatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa nchi zaidi ya 30 pamoja na mawaziri 80 wa wizara ya mambo ya nje na ulinzi pamoja na maafisa kadhaa.
Mkutano huo unafanyika mnamo wakati Rais Trump akiwa tayari ametoa kauli kadhaa kuhusiana na Jumuiya hiyo ya kujihami ya nchi za magharibi na hivi karibuni akitoa kauli inayooonyesha kukubaliana na umuhimu wa ushirikiano huo wa kijeshi. Hata hivyo, amesisitiza juu ya haja ya kila nchi mwanachama wa ushirikiano huo kulipa gharama sawa zinazohusiana na masuala ya ulinzi jambo ambalo viongozi wa NATO wamekuwa wakilipigania kwa muda mrefu.
Friday, 17 February 2017
MKUTANO WA AMANI WAANZA MUNICH
Unknown
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment