Mganga mmoja wa kienyeji huko jijini anashikiliwa juzi baada ya kumuingilia kimwili mgonjwa wa akili aliyekuwa anamtibu nyumbani kwake,mganga huyo wa kienyeji amekuwa na utaratibu wa kuwatibu wagonjwa mbalimbali.
Mgonjwa huyo aliletwa nyumbani kwa mganga huyo baada ya ndugu zake kumsafirisha kutoka nyumbani Kahama mkoani Shinyanga kwani sifa za mganga huyo kuhusu tiba zilisikika maeneo mengi. Ndugu wa mgonjwa huyo walimleta na kurudi nyumbani Kahama ili waweze kwenda kujipanga namna ya kupata fedha za kulipia gharama za matibabu pia hata chakula lakini baada ya kurudi ndugu hao kwa mganga huyo aliwaeleza juu ya kitendo alichofanyiwa na mganga huyo na kwenda kuripoti Polisi ambapo mgonjwa alienda kupimwa hospitali na kithibitisha kuwa alifanyiwa kitendo hicho.
Watu wengi hasa maeneo ya mikoa ya Kanda ya ziwa wamekuwa na utaratibu wa kupeleka wagonjwa wao katika tiba mbadala kwa ajili ya kutibiwa wakiamini kuwa maradhi mengi yanaletwa na kurogwa. Dhana hizi zimekuwa zikiendelea miaka hadi miaka na kupelekea kuongezeka imani za kuua wazee kwa mapanga.
Mganga huyo anaendelea kushikiliwa na Polisi na atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.
Saturday, 18 February 2017
MGANGA WA KIENYEJI AMBAKA MGONJWA WA AKILI MWANZA
Unknown
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment