Askofu wa Kanisa la ufunuo na uzima kanena yake ya moyoni leo akiwa kanisani kwa waumini wake,pitia mwenyewe uone alichosema
Askari walipekuwa nyumba yangu chumba hadi chumba lakini hawakukuta kitu chochote. Askofu Gwajima: Polisi wale hawawezi kuzungumza sababu wataonekana ni waasi. Mimi namuomba Rais aingilie kati hili suala watu wanateseka.
Lengo la Paul Makonda ni kuchafua majina ya watu kwa sababu anazozijua mwenyewe. Sijawahi kuvuta sigari, kunywa pombe wala kwenda disko tangu nimezaliwa mimi.
Mimi nitawaambia kitu, msilaumu Polisi wala Ofisi ya Rais. Wao hawahusiki na hili ila ni kiumbe mmoja tu ameibuka katikati.
Polisi nao wanateswa kama tunavyoteswa sisi. Wanaambiwa wakapekuwe nyumba yangu japo wanajua hamna kitu ila inabidi waende.
Kamanda Sirro akaniuliza kwa nini nimewekwa kwenye orodha hiyo, nikamwambia ni chuki tu za mtu aliyekaa kwenye kiti chake.
Waliniambia wakanipime kwa Mkemia na walinipima kwa uwazi kabisa. Niliwaambia hata wakikuta pombe wasema ni dawa za kulevya. Baada ya kukosa walichokuwa wanatafuta nyumbani kwangu tukarudi polisi usiku ule ule kuendelee na mahojiano.
Chumba nilichowekwa polisi nilikuwa mimi na manji. Nikasema 'kumbe na mimi nina pesa kiasi hiki hadi nawekwa na huyu?' Manji ana kampuni 23, na ameajiri watu zaidi ya 5000. Unashindwaje kumpelekea hati ya kumuita umhoji kabla ya kumtangaza?
Sheikh Mkuu na yeye badala ya kutetea taratibu zifuatwe anamuunga mkono swaiba wake, wanampango gani hawa?
Mimi ninajua chakumfanya Makonda, mapepo yaliomba kuingia kwa nguruwe, ila sasa nitayaambia pakwenda maana nguruwe ni nyama.
Mapolisi 12 wamewekwa kule ndani wamejikunyata hawana mtetezi, eti Makonda ameunda tu, yani kesi ya ngedere iko kwa nyani!!
Lengo la Paul Makonda ni kuchafua majina ya watu kwa sababu anazozijua mwenyewe.
Kwanini kina Manji wao hadi leo hawajafanyiwa kama nilivyofanyiwa mimi ili nao watoke mule ndani?
Unawaita watu waje wakuone, hata kama walikuwa na madawa si wataficha. Ndio maana nasema juhudi hizi si za dawa za kulevya.
Namuomba Rais Magufuli asiache kuamini vijana kwa sababu ya huyu mmoja, kichaa aliyeharibu. Wapo vijana wenye akili nzuri.
Rais Magufuli vita ya dawa za kulevya isikome lakini njia hii iliyotumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam si sahihi, ni ya ovyo na ya kijinga
Vitu vingine huhitaji kufundishwa darasani, ni akili za kawaida tu unatakiwa kuwa. Namuomba Rais awaangalie wale walioshikiliwa kule mahabusu, nimewaacha hawana mtetezi, kama wanakosa hatua zichukuliwe.
Kesho nitarudi tena kuwaona wale watu niliowaacha. Ninaamini sasa rais anahitaji msaada wangu. Mimi sikubali kama Makonda ataendelea kuwa Mkuu wa Mkoa.. Hana uwezo na hafai kabisa kwa nafasi hii
Hii vita imemshinda Makonda labda akipelekwa CCP anaweza akafaa kuwa Polisi. Kuanzia sasa mtu yeyote akiona jambo halipo sawa aniambie nitapaza sauti itapita mageti yote Kuanzia sasa mtu yeyote akiona jambo halipo sawa aniambie nitapaza sauti itapita mageti yote hadi kumfikia rais na atatenda... Hatuwezi kuongozwa na vichaa kama huyu Makonda
Makonda ni kombora ambalo halijaelekezwa pakutua, linaweza kutua sehemu yoyote.
Rais Magufuli ana hekima, anaweza akaona kitu hakipo sahihi lakini akakaa kimya akuone mwisho wako, au nani amekutuma.
Mimi umenitangaza, ukakuta sina dawa za kulevya, kesho ukiniita kwako usifikirie nitakuja, nitakuaminije?
Mimi ni kama mbegu, ukinifukia ukienda ukirudi unakuta ni mti umechanua vizuri na una matunda. Mamlaka aliyopewa Makonda si sahihi, nawaomba msikubali Makonda aendelee kuwa Mkuu wa Mkoa, lakini msifanye fujo. Rais Magufuli tunakuunga mkono kabisa kwenye vita dhidi ya dawa za kulevya, lakini njia aliyoitumia Makonda si sahihi.
Taasisi nyingine za serikali kama DCI, Mawaziri, Polisi hawathubutu kuongea sababu ya "Makonda Syndrome."
Mamlaka aliyopewa Makonda ni makubwa na matumizi yake mabaya. Nimepigiwa simu na viongozi wengine wakinipa pole na mmoja wao aliyenitumia 'msg' ni Dkt Slaa.
Hayo ndio aloyasema Askofu Gwajima.
Sunday, 12 February 2017
MCHUNGAJI GWAJIMA ANENA YA MOYONI JUU YA MAKONDA
Unknown
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment