Propellerads
Propellerads
Propellerads
Daily Updates!

We share informations with you

Propellerads

Wednesday, 15 February 2017

MASHAHIDI WA SERIKALI WAWEWESEKA KESI YA UCHOCHEZI YA TUNDU LISSU

Kesi namba 208 ya 2016 imekwama kuendelea leo katika Mahakama ya Kisutu baada ya Wakili kuhoji shahidi asihojiwe mambo ya Zanzibar.

Shahidi wa kwanza upande wa serikali alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Salumu Hamduni.

Wakili wa serikali Paul Kadushi aliiomba mahakama izuie lakini Lissu akijitetea alisema suala hilo lazima lijadiliwe sababu serikali yenyewe ndio imeliweka kwenye hati ya mashtaka.

Kesi inayomkabili Mwanasiasa Tundu Lissu na waandishi wa Gazeti la Mawio ulipofika wakati wa maswali maswali mengine yalileta utata mpaka mengine kupingwa,sehemu ya mahojiano hayo:

LISSU; Mikusanyiko isiyo rasmi, ni halali au sio halali

SHAHIDI: Ni halali

LISSU: Mihemuko na Hofu inazuiliwa kisheria?

SHAHIDI: Hapana

LISSU: Hofu kama ya Mungu, au ya shetani au ya Dikteta, inazuiliwa kisheria?

SHAHIDI: Ndio inazuiliwa,

LISSU: Sheria gani?

SHAHIDI: SIJUI.

LISSU; Mweleze hakimu, sisi tulikaa wapi kula njama ya kuchapisha gazeti hili

SHAHIDI: sijui

LISSU; Mweleze hakimu tuliwasiliana kwa njia gani ili kukaa pamoja kula njama kama tunavyoshtakiwa

SHAHIDI: Sijui

LISSU, unafahamu ni saa ngapi tulikula njama?

SHAHIDI: Sijui

LISSU; kabla ya kushtakiwa hapa je mimi nilifahamiana na washtakiwa hawawengine?

SHAHIDI; Sijui

Hakimu Thomas Simba aliahirisha kesi hiyo hadi kesho saa 3 na nusu.

0 comments:

Post a Comment

Propellerads