Kesi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, kampuni inayomiliki mtandao maarufu wa kijamii wa Jamii Forums, Maxence Melo imeahirishwa mpaka Machi 9 mwaka huu itakaposikilizwa tena
Kwa mujibu wa mtandao huo, kesi hiyo imeahirishwa kutokana na hakimu Mkazi Victoria Nongwa anayesimamia kesi hiyo kutokuwepo,hakimu huyo kwa udhuru alioupata siku chache kabla ya kusikilizwa kwa shauri lake.
Mkurugenzi huyo anakabiliwa na shitaka la kuendesha na kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa kwa anuani ya hapa nchini, kitu ambacho ni kinyume na sheria shitaka lingine ni kuzuia jeshi la polisi kufanya uchunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao pamoja na kusajili tovuti ya Jamii Forums kwa kikoa cha .com badala ya .co.tz jambo ambalo pia serikali inadai ni kinyume cha sheria.
Haya yote yanaletwa zaidi na ile sheria mpya ya makosa iliyoidhinishwa mwaka jana kuhusu mitandao na vyombo vya mawasiliano.
Thursday, 16 February 2017
KESI YA MEXENCE MELO WA JAMII YAPIGWA TAREHE
Unknown
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment