Mwanaume mmoja amehukumiwa miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji,ilikuwa ni mwaka jana mwezi June baada ya kumlaghai mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 24 kuwa amsindikize kwenda kuangalia majaruba eneo la Songe huko Musoma mkoani Mara.
Hakimu wa Mahakama hiyo Bwana Richard Maganga alilidhia ushaihidi uliotolewa mahakamani pasipo shaka kwamba bwana huyo alifanya kosa hilo ambalo liliamuachia maumivu makali kwani alifanyiwa tendo hilo kwa nguvu.
Mwendesha mashtaka aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine kwani matukio haya yamekuwa yakijirudia rudia kitendo ambacho kimekuwa si salama kwa jamii,nae mtuhumiwa alioomba Mahakama impunguzie adhabu kwani anategemewa na familia yake na akifungwa haitakuwa na mtu wa kuisaidia.
Wednesday, 22 February 2017
AHUKUMIWA MIAKA 30
Unknown
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment